RAIS KENYATTA ARIDHISHWA NA KIBARANI

Rais Uhuru Kenyatta ameelezea kuridhishwa kwake na shughuli inayoendelea yakuboresha bustani ya Mama Ngina kuwa bustani ya kisasa,pamoja na kupambwa na kadhalika kuboreshwa kwa eneo la kibarani.

Rais aliandamana na gavana Ali Hassan Jogo kutembelea mradi huo wa shilingi milioni 460 aliouzindua rasmi mwezi Januari mwaka huu.

Mabadiliko ya eneo la bustani ya Mama Ngina ni katika kjuhudi zinazoendelea za kuirudisha Mombasa kuwa jiji linalongoza kwa utalii katika kanda hii.

Kwa muda wa miaka mine eneo la kibarani limekuwa kero na wasi wasi kwa afya ya umma kwa wakaazi na wageni wanaoingia Mombasa.

Total Views: 41 ,