Rais amteua Fatuma Ahmed mwanamke wa kwanza kuhudumu kama meja generali katika jeshi la Kenya

Afisa wa ngazi ya juu zaidi mwanamke jeshini Brigedia Fatuma Ahmed amepandishwa ngazi na kuapishwa kuwa meja Generali ambapo ni mwanamke wa kwanza katika historia ya Kenya kupanda katika wadhfa huo.

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi wakati wa hafla ya kuapishwa kwake,rais Uhuru Kenyatta amemtaka afisa huyo ambaye pia ndiye wa kwanza kupata wadhfa wa ubrigedia mwaka wa 2015 kuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake wengine jeshini.

Rais Kenyatta aidha amemteua kamanda wa jeshi la nchi kavu Lieuten generali Robert Kibochi kama naibu mkuu wa majeshi wadhfa uliokuwa ukishikiliwa na Lieuten generali Joseph Kasaon anayetarajiwa kustaafu baada ya kuhudumu tangu mwaka wa 2015.

Kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na waziri wa ulinzi Raychelle Omamo,mkuu wa majeshi Samson Mwathethe na makanda wanaostaafu rais pia alimteua meja generali Walter Koipaton kuongoza jeshi la nchi kavu na meja generali Francis Ogola wa jeshi la Angani.

Mwisho

Total Views: 271 ,