Rais aahidi kuimarisha zaidi huduma ya polisi nchini

Rais  Uhuru Kenyatta ameahidi kutoa rasilmali zaidi katika mpango wa kuimarisha huduma ya taifa ya polisi ili kuiwezesha huduma hiyo kukabiliana na vitisho vya aina zote vya usalama wa kitaifa.

Akiongea wakati alipoongoza gwaride la kuhitimu kwa makurutu 3,984 wa polisi wa utawala katika chuo cha utoaji mafunzo kwa maafisa wa polisi huko Embakasi, rais alisema mpango huo unaojumuisha utoaji wa magari ya kutosha , silaha za kisasa  , magari yenye silaha ili kutumiwa kwa operesheni maalum na kukarabati kitengo cha ndege za polisi utaongeza mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya shughuli za uhalifu hapa nchini.

Rais ametoa wito kwa umma kuunga mkono mpango huo wa mashirika mbali mbali ambao alisema utasaidia Kenya kupiga hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi.

Amewataka maafisa wa polisi kuwa wazalendo na kutekeleza majukumu yao kwa ujasiri katika juhudi za kuwalinda wakenya.

Waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiang’i ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema mageuzi yanayojumuisha mtaala mpya wa utoaji mafunzo kwa polisi yataendelea.

Mwisho

Total Views: 181 ,