Raila Odinga akutana na rais Mstaafu Daniel Arap Moi

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amemtembelea rais mstaafu Daniel Arap Moi nyumbani kwake Kabarak.

Kulingana na hatibu wake, Denis Onyango,Raila alimtembelea rais huyo wa zamani ili kumtakia heri njema baada ya kuwa hospitalini nchini Israel ambapo pia wamezungumzia hali ya nchi wakati wa ziara hiyo iliyodumu kwa zaidi ya saa moja.

Onyango aidha amesisitiza kuwa rais huyo mstaafu ni mwenye afya njema na mkakamavu baada ya matibabu hayo ya goti aliyopokea mwezi jana nchini Israel baada ya kuhusika kwenye ajali tarehe 30 mwezi Julai mwaka wa 2006 katika eneo la Limuru.

Ziara ya Raila inajiri majuma kadha baada ya kukubali kufanyakazi na rais Uhuru Kenyatta kwa lengo la kuiunganisha Kenya kufuatia mgawanyiko uliojiri kwa msingi wa kisiasa baada ya kushuhudiwa kwa kipindi kirefu cha uchaguzi.

Mwisho

Total Views: 154 ,