Raila atamatisha ziara yake ya Mangharibi mwa Kenya

Kinara wa Cord  Raila Odinga, amekamilisha ziara yake ya juma moja magharibi mwa Kenya huku akiwarai wakazii wa eneo hilo kusalia katika upinzani na kumuunga mkono kwenye uchaguzi wa urais wakati wa  uchaguzi mkuu ujao.

Hata hivyo ziara yake huko Mumias leo ilikumbwa na maandamano ambapo vijana waliitaka kampuni ya  Spectre International inayomilikiwa na familia ya  Odinga kulipa deni la shilingi milioni 300 linalodaiwa na kampuni ya sukari ya  Mumias.

Wandamanaji hao walidai kuwa  deni hilo limechangia pakubwa masaibu ya kampuni hiyo ya sukari.

Hata hivyo Raila alikanusha kuwa ana deni la kampuni ya sukari ya Mumias,akisema kampuni hiyo ilifilisishwa na usimamizi pamoja na siasa duni.

Mwisho

Total Views: 385 ,