RAILA AMSHAURI SAMBOJA

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amemhimiza gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja kuruhusu majadiliano kwanza na wawakilishi wake wa wadi kabla ya kuchukua hatua ya kulivunja bunge lake.

Akizungumza kwenye mkutano na wajumbe kutoka kaunti ya Taita Taveta, Raila aliwashauri kufanya majadiliano pia na bunge la senate kwenye harakati za kutafuta suluhu la utata walionao.

Gavana Samboja alitangaza uamuzi wake wa kulivunja bunge baada ya kukiuka kutia saini ya bajeti ya billioni 5.6 iliobuniwa na bunge la kaunti hiyo.

Kwa sasa gavana Samboja anaendelea kukusanya sahihi ili kutafuta uungwaji mkono wa kulivunja bunge lake.

picha hisani

Total Views: 22 ,