Raila akutana na Kibaki

Juma moja baada ya kinara wa upinzani Raila Odinga kukutana na rais mstaafu Daniel Arap Moi nyumbani kwake Kabarak,hivi leo amekutana na rais Mstaafu Mwai Kibaki katika eneo la Muthaiga jijini Nairobi.

Akiandamana na wakili Paul Mwangi,Raila amefanya mazungumzo na rais huyo mtsaafu na aliyekuwa mshirika wake katika serikali ya muungano ambapo ajenda ya mkutano huo wakushtukiza haikuwekwa bayana.

Mapema Raila alikutana na Gavana wa Nairobi Mike Sonko katika ofisi zake za Capitol Hill jijini Nairobi ambapo Sonko alimpongeza Raila kwa hatua yake ya kuamua kushirikiana na rais Uhuru Kenyatta kwa manufaa ya taifa hili.

Mikutano hii ya Raila inajiri mwezi mmoja baada ya kukubali kufanyakazi kwa pamoja na rais Uhuru Kenyatta katika jumba la Harambee jijini Nairobi kwa lengo la kuwaunganisha wakenya baada ya mgawanyiko wa kisiasa ulioshuhudiwa mwaka jana.

Mwisho

Total Views: 206 ,