Raila akashifu wizara ya elimu

 

Kinara wa CORD Raila Odinga  ameikashifu wizara ya elimu kwa kile anachokitaja kutofaulu kwa mikakati ya kuzuia wizi wa mitihani ya kitaifa na kutaja kama chanzo cha visa vya uchomaji shule vinavyoshuhudiwa nchini kwa sasa.

Odinga amesema mikakati iliyokuwa imewekwa  kukabiliana na visa vya wizi wa mitihani ilianza kutekelezwa bila ya kufanyika mahojiano ya kina kati ya washikadau wa elimu sawa na kuwatenga walimu na wanafunzi.

Miezi miwili iliyopita wizara ya elimu iliagiza kufutiliwa mbali kwa shuhuli za maombi pamoja na kutemebela wanafuzi ,  ambazo hufanyika kila muhula wa tatu shuleni hatua ambayo haikupokelewa vizuri na wazazi , wanafunzi na baadhi ya washikadau katika sekta hiyo muhimu nchini.

Wizara ya elimu pia iliweka sheria kuwa walimu  wasiwe shuleni wakati wa mitihani ya kitaifa agizo ambalo lilionekana kukinzana na uhalisia wa mambo ambapo awali walimu walikuwa shuleni wakati wa mitihani ya kitaifa.

Aidha Odinga  ameitaka serikali ya Jubilee kuvunja kimya chake kuhusiana na ongezeko la visa vya uchomaji shule ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa nchini.

Total Views: 327 ,