Raila ajiondoa uchaguzini

Mgombea urais wa muungano wa NASA, Raila Odinga, kujiondoa kutoka kwa uchaguzi wa urais, Odinga amejiondoa kutoka marudio ya uchaguzi wa urais tarehe 26 mwezi Oktoba.

Odinga ambaye aliandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, vinara wenza Musalia Mudavadi na Moses Wetangula aliwaambia wanahabari katika makao makuu ya muungano wa NASA ya Okoa Kenya kwamba uamuzi huo umetokana na kukataa kwa tume ya uchaguzi –IEBC kutimiza matakwa yao ambayo yalijumuisha kuondolewa kwa maafisa tisa wa tume ya IEBC.

Odinga kadhalika alilaumu serikali ya Jubilee kwa kurekebisha kwa njia isiofaa sheria za uchaguzi kwa uzingativu wa maslahi ya chama cha Jubilee.

Mwisho

Total Views: 275 ,