Raila Afichua ni kwa nini hakumshirikisha Kalonzo kwenye ushirika na rais Uhuru

Kinara wa Upinzani Raila odinga hatimaye amefichua sababu zilizopelekea kumuacha nje mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka na vinara wenza wa muungano wa NASA kwenye mazungumzo yake ya ushirikiano na Rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza kwenye hafla eneo la Kitui Raila amesema kuwa kulikuwako na makubaliano ya pamoja na rais Uhuru Kenyatta kuhusu njia ya kuliunganisha taifa na kwamba hakuhitaji msukumo wa wendani wake wa kushinikiza swala hilo.

Raila amesema kuwa Kenya haijajikwamua kutoka kwa vifungo kwa mujibu wa malengo ya waanzilishi wa taifa hili hatua inayohitaji umoja na kusudi miongoni mwa viongozi kutoka kwa mirengo yote ya kisiasa.

Kadhalka Gavana wa Kitui Charity Ngilu ameelezea haja ya muungano wa NASA kusalia pamoja huku akitoa wito kwa uongozi wake kumuunga mkono Kalonzo Musyoka kuwania urais mwaka wa 2022.

Mwisho

Total Views: 136 ,