Pwani kushuhudia upepo mkali yasema idara ya utabiri wa hali ya anga

Idara ya utabiri wa hali ya hewa humu nchini, imetoa tahadhari juu ya uharibifu ambao huenda ukatokana na pepo kali zitakazovuma kwa kasi ya  mita 20 kwa sekunde katika muda wa siku nne zijazo. 

Kulinghana na idara hiyo, Upepo mkali unatarajiwa kukumba baadhi ya maeneo ya Pwani kuanzia leo hadi Jumamosi.

Idara hiyo inasema maeneo mengine yatakayoathiriwa na hali hiyo ni yale ya Kaskazini Magharibi, Kaskazini Mashariki na pia Mashariki mwa nchi.

Idara hiyo imetoa tahadhari juu ya uharibifu utakaoshuhudiwa kwenye kaunti za Lamu, Kilifi, Mombasa, Kwale na Tana-River; Kitui, Garissa, Isiolo, Wajir, Marsabit, Samburu, Turkana pia Mandera.

Wakaazi wa maeneo hayo wameshauriwa kuwa waangalifu.

Mwisho

Total Views: 149 ,