Pwani FM Yanyosha mkono wa Eid Kaunti ya Kwale

Pwani FM imewanyoshea mkono wa Eid waumini wa dini ya Kislamu katika eneo la Tiribe kaunti ya Kwale kama hatua moja ya kuwanonyesha upendo kwa jamii zinazohitaji msaada.

Ismail Mohammed mmoja wa waliofadika anasema, Pwani FM ndio kituo cha kwanza kuwaonyeshea mkono kwa kuwapa chakula huku akielezea kuwa idadi ya haja katika eneo hilo wanahitaji msaada wa chakula.

Zaidi ya familia 100 zilipata pakiti ya unga, mchele na mfuta.

Mfungo wa Ramadhan ni mojawapo ya nguzo muhimu katika dini ya kislamu.

Meneja wa kituo cha radio cha Pwani Fm Maximillah Walukhu  amesema kituo hiki kinajukumu la kutoa mchango wake katika kutatua baadhi ya matatizo yanayoikabili jamii ya eneo la Pwani.

Bi. Walukhu asema wataendelea kushirikiana na jamii  na washikadau wengine kutatua baadhi ya matatizo yanayowakumba wakaazi wa eneo la Pwani.

Total Views: 285 ,