PSG yamvutia Sanchez!!!

Huku mkataba wa Sanchez raia wa chile ukikaribia kutamatika ugani emirates mwishi mwa msimu huu, vilabu vya Real Madrid,Mancity, Bayern Munich na PSG ya ufaransa vipo mbioni kutwaa huduma zake.

PSG wapo tayari kumlipa sanchez kima cha Euro milioni 10m kama bonus kutokana na kutia sahihi kutua Parc des Princess sawa na kumlipa kima cha £275,000 kwa wiki.

Klabu cha arsenal kinapania kutwaa huduma za mchezaji Julian Draxler anayewajibikia PSG kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Sanchez. Huku hayo yakijiri usimamizi wa arsenal unapania kumwuza mchezaji Mesut Ozil kwa mabwenyenye wa hela ndefu nchini Italia , Intermillan.

Total Views: 190 ,