Producer Totti apinga madai ya msanii chipukizi kuwa abania track yake.

Producer wa KAY G records Totti amesema kuwa hajaibania track yake msanii toka kundi la Reclam Shyman.

Awali Shyman alikuwa amedai kuwa alikuwa amemaliza kurekodi track yake chini ya producer Totti na kulipa fedha zote walizokuwa wameelewana naye kukamilisha kazi yake.

Tulipomtafuta producer Totti kuhusiana na madai haya ya kusema.

“Nimekuwa na projects kadha ambazo nimekuwa nafanya hivi karibuni , ni kweli kuwa Shyman anatrack alioifanya chini yangu. Si eti nimeibania hio track , sababu kuu inayofanya ni kuwa kama wiki mbili zilizopita nimekuwa na shughuli za kukamiliasha video ua Kasaga” alisema Totti

Vilevile Totti alieleza kuwa kuna kazi za wasanii wengi ambazo pia zimesimamaishwa akitaja kazi mpya yake susumila na nyingine toka kwa 22 Mwangi.

“Kwa sasa naeza mweleza Shyman awemtulivu baada ya hizi kazi ambazo nazifanya kwa sasa ntakamilisha kazi yake” alisema Totti

 

 

Total Views: 772 ,