Polisi Wawasaka Washukiwa Wengine wa Mkasa wa Riverside Drive

Polisi wanaendelea kuwasaka washukiwa zaidi wanaoaminika kushiriki katika kupanga shambuzili la kigaidi eneo la Riverside Drive baada ya washukiwa  wengine 9 kukamatwa jana alhamis.

Idadi ya washukiwa hao imefikia 11 kufikia sasa ambapo Ali Salim Gichunge anashukiwa kuwa  mshiriki mkuu na ambae awali alisemekana kuuwawa wakati wa shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 21.

Gichunge ambaye  pia anafahamika kama Farouk kutoka Isiolo ndiye mumiliki wa nyumba eneo la Ruaka ambayo ilivamiwa na maafisa wa polisi muda mfupi baada ya shambulizi hilo ambapo yuko kizuizini pamoja na mkewe Wanjiru alias Kemunto.

Total Views: 78 ,