Polisi wawajibikie vilivyo visa vya kutoweka kwa wananchi lasema shirika la HRW

Watu-34 wametoweka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita hususan wakati wa oparesheni dhidi ya ugaidi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la Human Rights Watch, wengi wa waathiriwa hao walitoweka jijini Nairobi na katika eneo la Kaskaizni Mashariki.

Akizindua ripoti hiyo, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Kenneth Roth alisema wakazi wa eneo la Kaskazini Mashariki wanapaswa kulindwa dhidi ya mashambulizi yanayotekelezwa na wanamgambo wa Al-Shabab na sio kudhulumiwa na maafisa wa serikali.

Roth alisema polisi hawajachunguza kwa kina visa vya kutoweka kwa watu hao.

Mwisho

Total Views: 342 ,