Polisi Wanasa Washukiwa Zaidi wa Mkasa wa Dusit

Idara ya  polisi inasema kuwa washukiwa kadhaa wa ugaidi wamekamatwa katika kambi ya wkimbizi huko Dadaab,wakati wa oparesheni ya kuwasaka wahusika wa shambulizi la Dusit huko Nairobi.

Inspekta generali wa polisi Joseph Boinnet anasema kuwa mmoja wa wshukiwa hao alikuwa na pasi mbili za usafiri za kigeni.

Boinnet ameongezea kuwa washukiwa hoa watachunguzwa kuhusiana na ugaidi,japo hajasema iwapo wanahusishwa na shamblizi hilo la Riverside.

Total Views: 74 ,