Polisi Wafunzwa na Wanywaji Pombe

Maafisa wa polisi huko Pennsylvania wamekuwa na kibarua si haba cha kuwakataza raia dhidi ya kuitikia mwito wao wa hapo awali wa kuwataka wahisani wa unywaji pombe kupindukia kwa lengo la kuwapa maafisa wa polisi mafunzo.

Idara ya polisi basi iliweka wito huo kwa mtandao wa Facebook huku wakiwataka watu watatu pekee ambao wangetakiwa kubugia pombe kali na kwa wingi kwa lengo la kutoa mafunzo kwa polisi kubaini kiwango cha waliokunywa pombe .

Japo waliweka masharti ya wahisani kuwa na ripoti nzuri ya afya, na vile vile  kutokuwa na ripoti ya kuhusika katika visa vya uhalifu na utumizi mbaya wa dawa za kulevya, watu wengi walijitokeza kinyume cha matarijio yao.

Na si hayo tu taarifa iliyowekwa mtandaoni ilisambazwa maarufu shared 1,400 na walipata zaidi ya comments elfu tano ili mradi walitaka tu wahisani watatu pekee.

Picha: Wahisani

Total Views: 91 ,