Polisi Uchina Wamkamata baba Aliyemuachia Mwanawe Kuendesha Gari

Polisi nchini Uchina wamefanikiwa kumnasa baba wa mvulana wa umri wa miaka saba baada ya kumuachia  malaika huyo kuendesha gari kwenye barabara kuu.

Jamaa huyo aliweka video ya sarakasi hiyo kwenye mtandao wa kijamii iliyomuonyesha akiwa amebeba kijana wake miguuni na kumuachia kuendesha gari.

Video hiyo pia inaonyesha mvulana huyo akiwa amejawa na uoga na kumuita mara kadhaa huku babake akimshinikiza kuendesha gari na pia anasemekana alimuacha mtoto huyo kutoa kichwa chake nje.

 Alifuta video hiyo baada ya dakika 30 alipokashifiwa na watu kwenye mitandao ya kijamii  lakini polisi walifanikiwa kumpata na kisha kumtoza yuani 300 sawa na shilingi elfu 4300 za Kenya na kufutiia mbali leseni yake.

Total Views: 21 ,