Polisi Aliyemtishia Mshukiwa na Nyoka Kuchukuliwa Hatua za Kisheria

Imewalizimu maafisa wa polisi huko Indonensia kuomba msamaha na kuahidi kuchukuwa hatua za kisheria dhidi ya afisa moja wa polisi anayedaiwa kutumia nyoka kumshawishi mshukiwa wa wizi wa simu kukubali mashataka aliyokuwa anakabiliana nayo.

Kulingana na video iliyosambazwa kwenye mtandao kwenye video, afisa wa polisi anaonekana akimuzungusha zungusha nyoka kwenye shingo lake huku akimtaka mshukiwa aseme ametekeleza wizi mara ngapi

Mshukiwa aliyekuwa ameogopa sana alionekana akijibu mara mbili tu huku afisa wa polisi akimuamuru kufungua macho na mdomo na kutishia kutumbukiza nyoka kwenye mdomo wake.

Kitendo hicho kimezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii na kumlazimu afisa mkuu wa Polisi Tonny Ananda Swadaya kuomba msamaha na kukanusha kuwa kisa kingine kama hicho hakijaripotiwa baada ya wanaharakati wa kutetea haki za kibnadamu kudai kuwa mwenzao alitishiwa vivyo hivyo.

Total Views: 69 ,