Pigo kwa Man City- De Bruyne nje wiki 4

Klabu ya Manchester City imepata pigo baada ya nyota wao Kevin De Bruyne kuthibitishwa kuwa atakuwa mkekani akiuguza majeraha kwa muda wa majuma 4.

Mchezaji huyo raia wa Belgium mwenye umri wa miaka 25 alipata jeraha la Paja wakati wa mechi kati yao na klabu Swansea City mechi ambayo walishinda mabao 3-1 katika uga Liberty Stadium siku ya Jumamosi.

De Bruyne amekuwa nguzo muhimu katika mechi zote 10 Mancity iliyoweza kupiga msimu huu chini ya meneja mpya Pep Guardiola

Total Views: 477 ,