Picha ya watu 500 wa Familia moja

Msikilizaji, amini usiamini, familia moja nchini Uchina hatimaye imetimiza ndoto na kupigwa picha ya watu 500 wa familia hiyo.

Inasemekana kuwa wakati wa kusherehekea mwaka mpya nchini humo , familia ya Ren kutoka kijiji cha SHISHE  ilitafuta vizazi saba na kufaulu kuwapata watu 500 na kufanya sherehe  ya kuwaleta pamoja na kisha kupiga picha kwa pamoja.

Mpiga picha Zhang Liangzong asema familia hiyo inakisiwa kuwepo miaka 851 iliyopita na walifaulu kuwapata wanafamilia 2000 lakini 500 pekee walipatikana kwa sherehe hiyo pamoja.

Wazee kijijini humo pia wameanza harakati ya kutafuta vizazi vyao ili kuweka sawa rekodi za familia.

Total Views: 418 ,