Panyako Atishia Kuendelea kwa Mgomo wa Wauguzi

Muungano wa wauguzi nchini umesisitiza kuwa mgomo wa wauguzi ulioanza leo utaendelea ikiwa serikali haitaafikiana na wauguzi hao.

Katibu mkuu wa muungano huo Seth Panyako amesema kuwa njia pekee ya kumaliza mgomo huo ulioathiri kaunti 11,ni wauguzi walipwe.

Akizungumza huko mjini Eldoret Panyako  amedai kwamba waziri wa leba Ukur Yattani,amekuwa akipuzilia mbali malalamiko yao tangu walipotoa ilani ya mgomo huo Novemba,2018.

Kwa upande wake Yattani amewataka wauguzi kusitisha mgomo huo.

Wauguzi wanaitaka wizara ya afya kutekeleza mkataba wa pamoja wa maelewano wa mwaka 2017.

Total Views: 95 ,