Omtatah aitaka mahakama kuwalazimisha makamishna wa IEBC waliojiuzulu kuondoka ofisini

Mwanaharakati Okiya Omtatah anataka makamishna watatu wa tume ya uchaguzi IEBC waliojiuzulu juma lililopita kufanya hivyo rasmi sawia na kupeana rasilimali za umma zilizo chini ya usimamizi wao.

Kwenye kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya Leba,Omtatah anahoji kuwa hatua ya watatu hao kutojiuzulu rasmi inasababisha ugumu kwa tume ya IEBC kutangaza nafasi zao kuwa wazi kwa lengo la kuanzisha mikakati ya kuzijaza.

Anadai kuwa naibu mwenyekiti Consolata Maina,Kamishna Paul Kurgat na Margaret Mwachanya hawakufuatilia tangazo lao kwa umma kwa kuwasilisha barua zao za kujiuzulu kwa rais Uhuru Kenyatta au kwa tume hiyo.

Omtatah anasisitiza kuwa ni kinyume cha sheria kwa watatu hao kuendelea kupokea mshahara na manufaa mengine licha ya kuwa hawaihudumii tume hiyo tena ambapo ameitaka mahakama kuwalazimisha kuondoka ofisini.

Mwisho

Total Views: 187 ,