ODM yapongeza hatua ya Raila kukutana na rais Uhuru

Chama cha ODM kimepongeza mkataba wa kisiasa ulioafikiwa siku ya Ijumaa baina ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama hicho  Raila Odinga.

Haya yalijiri baada ya vinara watatu wenza wa NASA Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula kukutana na Raila kuhusiana na mkataba huo wa umoja na rais.

Akiongea leo baada ya kuhudhuria mkutano wa wabunge wa chama hicho katika jumba la Orange ulioongozwa na katibu mratibu Junet Mohamed alisema kuwa wanaunga mkono kikamilifu mkataba huo.

Junet alisema kuwa wabunge hao wamemhimiza kiongozi wa chama chao kuendelea kupigania Kenya bora yenye haki, inayowahusisha wote na yenye usawa.

Mwisho

Total Views: 118 ,