OCPD WA MALINDI MATAWA MUCHANGI AFARIKI

OCPD wa Malindi Matawa Muchangi ameaga dunia mapema leo katika hospitali moja mjini Mombasa.

Kulingana na mratibu eneo Pwani John Elunguta,mwenda zake alikuwa akiugua kwa muda kabla ya kufariki alipokuwa akipokea matibabu.

Elungata amesema kuwa marehemu alianguka nyumbani kwake kabla ya kukimbizwa hospitalini.

‘’Amefariki usiku wa kuamkia leo na tunasikitika sana ,wajua huwezi kuzuia kifo na OCDP amekuwa akiugua kidogo lakini tulidhania ameimarika lakini amepatwa na pressure na akaanguka sasa huko kuanguka ndio kulimuumiza sana’’

Elunguta amemtaja marehemu kama afisaa aliyejitolea kazini na kuwataka maafisa wengine kumuiga

Total Views: 106 ,