Ochomo Aondoka Muhoroni….

Mshambulizi matata katika klabu ya Muhoroni youth Wycliff Ochomo amekatiza mkataba wake na klabu hiyo kutokana na kile anachokitaja unyanysaji kutoka usimamizi wa klabu hiyo.

Hivi majuzi Ochomo alisimamishwa kazi klabuni humo , huku mwenyekiti wa Muhoroni Youth Moses adagala akisema utovu wa nidhamu ndio ulichangia hatua hiyo.

Ochomo mwenye umri wa miaka 31 ndie mfungaji bora katika ligi kuu ya kitaifa akiwa na mabao 12.

Total Views: 351 ,