Ochillo Ayacko Ashinda kiti cha Useneta Migori

Ochillo Ayako ameshinda kiti cha useneta kaunti ya Migori kwa kura 85,234 (57.7%) huku mpinzani wake wa karibu Eddy Oketch wa chama cha Federal akipata kura  60,555 (40.99%).

Waziri huyo wa zamani ambaye alikuwa akiwania kupitia tiketi ya chama cha ODM alichukuwa uongozi wa mapema tangu jana jioni baada ya kupata matokeo kutoka maeneo bunge 4 kati ya 8.

Uchaguzi huo mdogo ulishuhudia idadi ndogo ya wapiga kura ambayo ilikuwa asilimia 38 katika kaunti hiyo yenye wapiga waliosajiliwa 388,633 ambapo katika shughuli hiyo kura 511 pekee ndizo ziliharibiwa.

Total Views: 152 ,