Oburu Odinga amjibu Duale,nina haki ya uteuzi wa aina yoyote

Mbunge maalum Oburu Odinga amekanusha madai kuwa ameteuliwa kama mwanachama wa bunge la Afrika Mashariki na chama cha ODM kama ilivyodaiwa hapo jana na kiongozi wa wengi bungeni Adan Duale.

Akizungumza hapa Mombasa, Oburu amemtaka Duale akome kumzushia maneno yasio na msingi akieleza kuwa alijiondoa katika uteuzi huo siku tatu zilizopita ili aweze kuwa na muda wa kutosha wa kumfanyia kakake Raila Odinga kampeni za ugombea urais.

Mwisho

Total Views: 310 ,