Nywele yenye Uzani wa 1.5Kg Yapatikana tumboni mwa msichana wa umri wa miaka nane

Madaktari nchini Uchina wamemfanyia msichana mmoja mwenye umri wa miaka minane upusuaji na kupata nywele yenye uzani wa kila moja na nusu tumboni.

Mamake malaika huyo amefichua kuwa binti yake  amekuwa akila nywele zake tangu akiwa na miaka miwili.

Mama huyo anasema alianza kuwa na wasiwasi pale tumbo lake lilipoanza  kufura na kisha kuambatana na maumivu.

Alimpeleka hospitali na kisha madktari kumfayia upusuaji na kupata nyewele yenye uzani wa kilo moja na nusu ikiwa imezingirwa na chakula.

Madkari wanasema hali ya kuwa na msukumo wa kula nywele inajulikana kama Pica na hata huenda waathiriwa wakavutiwa kuanza kula vifaa  vingine.

Total Views: 205 ,