NTSA yauonya umma dhidi ya kushambulia maafisa wake

 

 

 

Mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA imeuonya umma dhidi ya kuwashambulia maafisa wake wakati wa kuwasaka madereva wanaolewa na kuendesha magari.

Onyo hilo linajiri baada ya maafisa wa mamlaka hiyo kurushiwa mawe wakati wakitekeleza oparesheni sawa na hiyo jijini Nairobi,hatua ambayo mkurugenzi wakeFrancis Meja anasema haitavumiliwa.

Kadhalika Meja alitaja hatua hiyo kutokana na uamuzi wa wa mahakama ya rufaa ambayo ilisimamisha matumizi ya kifaa cha kupima kiwango cha pombe almaarufu Alchohol blower.

 

 

Total Views: 262 ,