NJAA LAMU

Zaidi ya wakaazi elfu 2 katika kijiji cha Pandanguo kaunti ya Lamu wanakabiliwa na uhaba wa chakula na maji.

Wakaazi hao wengi wao wakitoka jamii ya Boni , kwa miaka minnne iliyopita wamekuwa wakitegemea msaada wa chakula kutoka kwa serikali ya kitaifa na mashirika yasiokuwa yakiserikali.

Shughuli za jamii ya wa Boni ambao hutegemea sana  uwindaji zilisitishwa tangu mwaka 2015 baada ya serikali kuzindua oprasheni ya kuwasaka wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Shabab wanaoaminika kujificha katika msitu wa Boni al maaruf Linda Boni.

Juhudi za jamii hiyo kukumbatia ukulima kwa kutumia mbinu za kisasa zimeambulia patupu kufuatia hali ya kiangazi iliyokumba eneo hilo kwa muda sasa.

Mzee wa kijiji hicho Aden Golja anasema kwa sasa wanalazimika kula samaki tu ili kuuwa makali ya njaa.

 

Total Views: 74 ,