Mombasa:Ni lazima mauaji ya Kiholela yasitishwe asema Gavana Joho

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amekashifu vikali njia inayotumiwa na polisi kukabiliana na washukiwa wa uhalifu hapa Mombasa na Pwani yote kwa jumla.

Akizungumza kwenye makaazi ya mwendazake Salim Bedzimba katika eneo la Kisauni, Gavana Joho ameonya kuwa uongozi wa kaunti ya Mombasa pamoja na mashirika ya kijamii watapanga maandamano ya kukashifu mauaji hayo.

Kauli yake inajiri siku moja baada ya polisi kuwaua kwa kuwapiga risasi washukiwa watatu wa uhalifu katika eneo la kisauni akiwemo Salim ambaye ni nduguye mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba.

Mwisho

Total Views: 468 ,