Ndovu na Teknolojia

NDOVU 2Shirika la huduma kwa wanyama pori nchini (K.W.S) limeanzisha shughuli ya siku tatu ya kuweka vifaa vya uchunguzi kwenye ndovu kumi katika mbuga za kitaifa za wanyama pori za Tsavo magharibi na mashariki.

Naibu mkurugenzi wa hifadhi ya Tsavo Nahodha Robert O’Brien, alisema kuwa shughuli hiyo inalenga kuweka vifaa hivyo kwenye ndovu ambavyo vitakuwa vikiwasilisha ishara kwenye kituo kikuu ili kuifanya rahisi kwa walinzi wa KWS na kikosi cha kuwachunguza ndovu hao kufuatilia mienendo yao katika mbuga hiyo.

O’Brien alisema kuwa watakuwa wakiweka vifaa hivyo kwenye wanyama hao katika eneo la ziwa Jipe huko Taveta, karibu na barabara kuu ya Mwatate-Taveta pamoja na wale wanaoishi karibu na mradi unaoendelea wa ujenzi wa reli ya kisasa.

Mwisho

Total Views: 364 ,