NDOA CHANGA TANA DELTA

Polisi huko Tana Delta kaunti ya Tana River wamewakamata wanandoa wawili kufuatia kumuoza binti yao wa miaka 15 kwa mwanaume wa miaka 37.

Msichana huyo anasemekana kuolewa  punde tu baada ya kukamilisha mtihani wake wa  kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka jana kwa mwanaume ambae ni mwenyekiti katika shule moja ya msingi eneo hilo.

Wazazi wa mwanafunzi huyo, baba akiwa na umri wa miaka 46 na  mama wa umri wa miaka 34 walimuozesha binti yao baada ya kupokea  zawadi.

Naibu Kamishna eneo la Tana Delta Charles Akwanalo amesema baada ya kufanyiwa uchunguzi kadhaa wa kiafya ilibainika kuwa msichana huyo alikuwa amenajisiwa na mwanamume huyo.

Kwa sasa wawili hao watasalia korokoroni wakisubiri kufikishwa mahakamani huku baba ya mtoto akisisitiza kwamba ni lazima binti yake aolewe.

Total Views: 75 ,