NDETI APATA PIGO

Wavinya Ndeti amepatwa na pigo baada ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kufutilia mbali uteuzi wake kama mgombea wa kiti cha ugavana kwa tiketi ya chama cha Wiper.

Jopo la kusuluhisha mizozo la IEBC limefuta leo uteuzi wa Ndeti baada ya kubaini kwamba ni mwanchama wa vyama viwili vya kisiasa Wiper Democratic Movement na Chama Cha Uzalendo.

Hatua hiyo inajiri kufuatia rufaa iliyowasilishwa na mpiga kura kwa jina Kyalo Peter Kyuli ambaye pia ni mwanachama wa bunge la kaunti ya Machakos.

Kyuli alikua amelitaka jopo hilo kufutilia mbali uteuzi wa Ndeti na kubatilisha cheti chake alichokabidhiwa na chama cha Wiper.

Total Views: 325 ,