NCIC na mbunge mteule zataka wanasiasa wachochezi kuadhibiwa

Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC imetaka vyama vya kisiasa nchini kuwachukulia hatua kali za kisheria wanasiasa watakaopatikana wakichochea vijana kufanya vurugu au kujihusisha na semi za chuki.

Wakizungumza mjini Ruiuru mbunge mteule Isaac Mwaura na kamishna wa  NCIC profesa Naituli Gitile wamewaonya wanasiasa dhidi ya kuchochea wananchi wakati huu ambapo taifa linajiandaa kwa uchaguzi mku utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Akirejelea matukio ya hivi karibuni katika maeneo ya Gatundu kusini na na Busia ambako kulizuka vurugu za kura za mchujo,Mwaura ametaka vyama vya kisiasa kuhakikisha kura ya uwazi na haki ili kuhakikisha amani inadumu katika taifa hili.

Total Views: 267 ,