NASA yataka hatua kuchukuliwa dhidi ya baadhi ya makamishna wa IEBC

Muungano wa NASA umetaja hatua ya mahakama ya Kubatilisha uchaguzi wa urais kuwa uamuzi wa kihistoria na unaodhihirisha uhuru wa idara ya Mahakama.

Huku akiwapongeza mawakili kwa kufanya kazi nzuri, mgombea urais wa muungano wa NASA, Raila Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka walitaja uchaguzi mkuu uliokamilika hivi punde kuwa wa kilaghai.

Ametaka kuchukuliwa hatua za kisheria kwa baadhi ya makamishna wa tume ya IEBC.

Ekuru Aukot ambaye aliibuka wa tano kwenye uchaguzi wa urais na alijumuishwa kwenye rufaa hiyo alisema nchi hii kamwe haipaswi kubakia kama ilivyokuwa huku akihimiza kuwepo tume ya uchaguzi isioegemea upande wowote kusimamisha marudio ya uchaguzi.

Mwisho

Total Views: 219 ,