NASA yasitisha maandamano kwa mda, huku mahakama ikifutilia mbali marufuku ya serikali dhidi ya maandamano hayo

Kinara wa Upinzani Raila odinga ametengaza kusitishwa kwa maandamano dhidi ya tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Akizungumza mapema leo ,Raila amewataka wafuasi wake kutofanya maandamano hayo ya kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguzi ,ili kupeana nafasi ya kutoa heshima kwa wale waliofariki kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano hayo.

Amesema kuwa atapeana muelekeo kuhusu maandamano hayo siku ya sherehe za mashujaa ijumaa tarehe ishirini juma hili hatua inayojiri siku chache baada ya muungano huo kutangaza kufanyika wka maandamano kila siku ya juma.

Mapema leo mahakama ya juu iliondoa kwa mda marufuku ya maandamano dhidi ya IEBC katika miji ya Nairobi,Mombasa na Kisumu iliyokuwa imetangazwa na serikali hatua inayojiri kufuatia kesi iliyowasilishwa na afisa mkuu mtendaji wa NASA Norman Magaya.

Mwisho

Total Views: 207 ,