Naibu wa Rais awataka viongozi wa pwani kuzingatia maendeleo badala ya siasa

Naibu wa rais William Ruto ametoa wito kwa viongozi wa Pwani kushirikiana na serikali kwa manufaa ya wananchi kimaendeleo ikizingatiwa kuwa mda wa siasa ulikamilika.

Akizungumza katika shule ya msingi ya Kwa Jomvu hapa Mombasa wakati wa uzinduzi wa barabara ya Jomvu-Rabai,Naibu huyo wa rais amesema kuwa sasa ni wakati wa kuwafanyia kazi wananchi bila kujali mueleko wa kisiasa.

Aidha wabunge kutoka kaunti za pwani walioandamana na naibu huyo wa rais kwa sauti moja wameahidi kufanyakazi na serikali ili kuhakikisha kuwa mwananchi anafaidika kwa mujibu wa katiba.

Ruto yuko hapa Pwani kwa ziara ya maendeleo ambapo kesho atakuwa eneo la Msambweni kaunti ya Kwale kabla ya kutamatisha ziara hiyo siku ya jumapili katika kaunti ya Taita Taveta.

Mwisho

Total Views: 141 ,