Naibu wa rais asema serikali inatambua vilivyo juhudi za wakenya

Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa serikali inatambua majukumu muhimu yanayotekelezwa na watu binafsi nchini wanaojitolea kuwakuza vijana katika nyanja mbali mbali nchini.

Akizungumza katika ofisi zake za eneo la Karen jijini Nairobi, Ruto amesema kuwa kuna haja ya kufanyika kwa mipango zaidi ya kuwakuza vijana hasa mashuleni kwa lengo la kukabiliana na swala la wanafunzi kuzua vurugu.

Ametaja mpango huo kuwa suluhu mwafaka la kukabiliana na swala la ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi wanaochoma mabweni ikizingatiwa kuwa utawawezesha kufahamu lililo zuri na baya katika jamii.

Mwisho

Total Views: 362 ,