Nahofia Maisha Yangu asema muwakilishi wa wanawake kaunti ya Kilifi Bi Aisha Jumwa

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa anadai kuwa anahofia maisha yake baada ya kupokea simu anayodai ni ya kumtishia maisha.

Akizungumza na wanahabari Bi Aisha alisema kuwa alipokea simu hiyo mwendo wa saa nne asubuhi ya leo iliyomtaka kuelezea kwa nini alitumia neno “JAMAA” kumrejelea rais Uhuru Kenyatta.

Alisema kuwa aliyempigia simu alidai kuwa anamfuatilia shughuli zake jambo ambalo muwakilishi huyo wa wanawake anadai kumtia hofu na kumfanya kuamini kuwa maisha yake yamo hatarini.

Akizungumza kwa njia ya simu mwenyekiti wa GEMA, Crispus Waithaka alikanusha madai ya kumtishia maisha mwakilishi huyo wa wanawake na kusema kuwa alimtaka kuiomba radhi jamii ya wagema kwa kosa la kumwita rais “Jamaa”.

Juhudi zetu za kupata habari kutoka kwa idara ya usalama ziligonga mwamba kwani kamanda wa polisi wa kaunti hiyo alisema hakuwa amepata habari hizo.

Mwisho

Total Views: 1340 ,