MZOZO WA ARDHI MALINDI

Wakaazi wa kaunti ndogo ya Malindi katika kaunti ya Kilifi wanaishi kwa hofu ya kufurushwa na mabwenyenye wanaodai ardhi wanazoishi ni zao, ardhi ambazo wanadai wameishi kwa zaidi ya miaka 50.

Wakiongozwa na Karisa Mweni ambaye ni mzee wa mtaa wa Kwandomo eneo la Sabaki anasema kuna haja ya serikali kuingilia kati na washirikiane na serikali ya kaunti ili wahakikishe wakaazi wameandikishwa na kupewa hatimiliki za ardhi.
Kwa mujibu wa Mweni mara kwa mara wamekuwa wakitafuta usaidizi kutoka kwa viongozi walioko mamlakani lakini kufikia sasa juhudi zao hazijafua dafu.

Ruth Kaingu ni mmoja wa wakaazi wa Kibokoni eneo la Sabaki wanaoohofia kufurushwa na anaeleza masaibu yao.

picha hisani

Total Views: 16 ,