Mzee aliye na shule na soko lake

Hebu tafakari haya, uwe na watoto wengi hadi ulazimike kuwa na shule na hata soko lako.

Na haya hayafanyiki mbali bali ni hapa hapa nchi jirani ya Tanzania.

Mzee Meshuko Ole Mapi, almaarufu Mzee Laibon, amelazimika kuwa na shule yake na soko kwa ajili ya familia   yake. Mzee huyu wa miaka 100 ana  wake wanane na watoto zaidi ya 70 na wajukuu 300 hali iliyomchochea kuwa na shule na soko lake .

Na anasema ataendelea kuoa na kupata watoto.

Kulingana na shirika la BBC, Watu kutoka mataifa mbali mbali hufika kumtembelea mzee huyo kama sehemu ya utalii.

Total Views: 698 ,