Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi awaonya wanasiasa dhidi ya kuingilia shughuli za tume hiyo

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Wafula Chebukati amewaonya wanasiasa dhidi ya kuingilia maswala ya tume hiyo akisisitiza kuwa haitaruhusu usumbufu wowote wa kisiasa kutatiza matayarisho ya marudio ya uchaguzi wa urais.

Akizungumza na wanahabari saa chache baada ya Kamishna wa tume hiyo Bi Roslyn Akombe kujiuzulu kiwa nchini Marekani ,Chebukati ametaja muingilio wa kisiasa kama moja wapo ya changamoto zinazoikumba tume hiyo.

Aidha amedokeza kuwa hataendelea kuongoza tume iliyogawanyika katika msingi wa kisiasa akitaja matakwa ya wakenya kuwa maswala yanayostahili kupewa kipau mbele kwa kuwataka maafisa wanaotiliwa shaka maadili yao kujiuzulu.

Bi Akombe amejiuzulu akilalamikia ukosefu wa ushirikiano miongoni mwa makamishna wenzake sawia na vitisho dhidi ya maisha yake akisema kuwa tume hiyo haiwezi ikaendesha uchaguzi wazi,huru na wa kuaminika jinsi ilivyo.

Mwisho

Total Views: 186 ,