Mwanamziki Maarufu Afrika Kusini Afariki

Hugh Masekela,  mwanamuziki maarufu wa mtindo wa jazz kutoka Afrika Kusini  ambaye pia inatumbulika kama ‘baba wa Afrika Jaz’ afariki.

Mwanmziki huyo aliyechangia juhudi za kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo, amefariki dunia akiwa na miaka 78 baada ya kuugua saratani ya tezi dume kwa muda mrefu.

Masekela alibobea kutokana na mtindo wake wa kipekee wa Afro-Jazz na vibao vilivyokuwa maarufu kama vile Soweto Blues.

Wimbo huo ulitoka mwaka  1977 na kuchangia pakubwa katika  harakati za kupambana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

Masekela pia alimiliki tarumbenta yake ya kwanza akiwa na miaka 14.

Total Views: 255 ,