Mwanamume Anayekunywa Mkojo

Mwana mitindo wa mavazi mwenye umri wa miaka 34 nchini Marekani hunywa mkojo wake kila siku.

Fabian Farguharson amekuwa akinywa matone kadhaa ya mkojo wake kwa muda wa miaka mitatu sasa baada ya kufanya utafiti na kubaini kuwa mkojo una manufaa kiafya.

Mwanamume huyo anasema alipata msukumo huo baada ya madaktari kushindwa kubaini chanzo cha maumivu ya tumbo lake.

 Anadai kuwa tangu aanze kuunywa mkojo wake, anaendelea kupata nafuu .

Total Views: 460 ,