Mwanamume aliyekuwa Amefariki Hatimaye Afariki Tena

Mwanamume mmoja raia  wa Ethiopia ”aliyefufuka” wakati wa mazishi yake miezi mwili iliyopita amefariki  tena dunia.

Hirpha Negero alithibitishwa kufa mwezi Novemba ambapo aliwekwa ndani ya jeneza kwa saa tano, lakini wakati wa mazishi yake wanavijiji walisikia akigonga jeneza.

Sasa amekuwa gumzo mtaani, huku watu waliokuwa wakimfahamu wakitafakari jinsi alivyofufuka miezi miwili iliyopita na kuwacha kijiji kizima kwa mshangao.

Mchimba kaburi Etana Kena anasema mara hii alihakikisha bwana huyo amefariki kabisa ndiposa akamuzika huku akielezea kuwa hakutaka yale yalifanyika hapo awali kuruduliwa.

Hirpha aliambia shirika la BBC kuwa alijihisi  kuishiwa na pumzi ndiposa  akajaribu kujitoa katika hali hiyo huku akiwa  mnyonge na hata hakuweza kuzungumza.

Dkt Birra Leggese hata hivyo  ameiambia BBC, huenda Hirpha alipoteza fahamu vibaya sana maarufu kama  “deep coma” n

Lakini sasa, wanakijiji wanasema wanaamini amefariki kweli baada ya kuzikwa siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kifo chake bila kuona dalili zozote za kufufuka.

Total Views: 90 ,