Mwanamke Sydney Ataka Kutangazwa Muathiriwa wa Uhalifu wa Salamu Za Mkono.

Mwanamke mmoja jijini Sydney nchini Australia anataka atangazwe kuwa mwathiriwa wa uhalifu kuhusiana na salamu za mkono.

Mwanamke huyo amesema kuwa wakala mmoja wa nyumba za kupangisha alitekeleza uhalifu huo kwa kutumia nguvu zaidi alipomsalimia kwa mkono na hivyo kumjeruhi.

Mwanamke huyo alisema kuwa mkono wake wa kushoto ulifura na alikuwa na maumivu makali kwa miezi kadhaa.

Alisema alienda hospitalini na akapata tiba ya mazoezi ya mkono huo kabla ya kuripoti kisa hicho kwa polisi.

Alisema sasa anafaa kupata ushauri nasaha na ruzuku za kifedha.

Hata hivyo wakala huyo alisema alimsalimia mwanamke huyo kwa mkono kumuaga tu.

 

Total Views: 23 ,