Mwanamke anayejiita Mungu afyatua risasi na kuuwa

Polisi nchini India wanamtafuta Sadhvi Deva Thakur, mwanamke  anayejiita Mungu aliye mafichoni baada ya ya kumfyatulia  risasi shangaziye bwana harusi na kumua kwenye sherehe za harusi.

Watu watatu walijeruhiwa vibaya wakati wa tukio hilo.

Vyombo vya habari nchini India vinasema kuwa Sadhvi, ambalo ni jina la kiindi linalomaanisha mwanamke aliye mtakatifu au anajiita kuwa mungu alingia sakafuni, ambapo alimuomba DJ kucheza wimbo aliotaka na akaanza kucheza densi kabla kufyuatiliwa risasi.

Kwenye video ya tukio hilo lililotokea siku ya Jumanne katika jimbo la Kaskazini la Haryana, Sadhvi Deva Thakur alionekana  akifyatua risasi akitumia bunduki aina ya revolver.

Baadhi ya walinzi wake nao pia walionekana wakifyatua risasi.

Total Views: 531 ,